PRIME MINISTER / Waziri Mkuu Majaliwa kamsimamisha kazi Daktari kwa kuomba rushwa ya Laki moja …(+Audio) By Emmanuel TZA on March 1, 2016



PRIME MINISTER TO FIRE DOCTOR WHO IS ACCUSED OF CORRUPTION ABOUT 100,000 TSH

February 29 2016 stori kutokea Mtwara, ilikuwa ni hii ishu ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi mmoja wa  Madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Wilaya mkoani hapo.

Daktari huyo alituhumiwa kuomba rushwa ya Shilingi laki moja kutoka kwa mgonjwa, hatua hiyo ikampelekea pia Waziri Mkuu huyo kukasirishwa na kuagiza maduka yote ya dawa yaliyokaribu na hospitali hiyo kufungwa mara moja kutokana na madaktari kujihusisha na biashara hiyo na kuachana na dawa za Serikali.


Nani alitaka laki moja kutoka kwa mgonjwa?, simama mwenyewe.. ulimuambia kanunue dawa, dawa shilingi 80 unasema kanunue alafu leta laki moja, ameleta dawa unamwambia laki moja yangu iko wapi?’
Sasa naanza na wewe, unasimama kazi na uchunguzi uendelee, na wengine wote ntakao wabaini basi utaratibu ni huu
Unaweza pia Waziri Mkuu kumsikiliza kwenye hii sauti hapa…



Share on Google Plus

About Emmanuel

0 comments:

Post a Comment