Nahodha wa timu ya taifa ya TanzaniaMbwana Samatta April 16 2016 alipata nafasi ya kuanza na kucheza mechi kwa dakika 90 kwa mara ya kwanza akiwa na KRC Genk ya
Ubelgiji, Samatta ameanza na alifunga goli la uongozi kwa Genk dakika ya nane ya mchezo kwa mpira wa kichwa baada ya kutumia vyema krosi safi iliyotoka kwa nahodha wa GenkThomas Buffel. Genk imeibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Zulte-Waregen
0 comments:
Post a Comment